Wanaume wengi wanapobaini kuwa wapenzi wao wanawasaliti,
hutunisha misuli kuonesha umwamba kwa kuwatwanga makonde wapenzi wao au
kuwafanyia mbaya wale waliowanasa. Lakini uchunguzi wa wana mapenzi
unaonesha kuwa ubabe haukomeshi tabia ya usaliti.
Kuna wengi ambao waliwafumania wake zao, wakawapiga na
kuwajeruhi, lakini wakajikuta hawakukomesha tatizo, zaidi ya kuwapa
usugu wapenzi wao wa kuendeleza wizi tena kwa dharau na kejeli huku
wakibembelezana kwa maneno haya: “mzushi kaenda kazini njoo sasa hivi
Wapendanao Gesti” au “vipi yule bwege alikuuliza jana ulipochelewa
kurudi” Jamaa anaweza kumuuliza hivyo mke au mpenzi wa mtu.
Katika hali ya kawaida usaliti ni jambo linalouma kwa
kiwango kikubwa. Katika mapenzi hakuna suala la kuazimana mume/mke. Watu
huazimana magari na pesa, lakini laazizi hakuna jasiri wa namna hiyo!
Hivyo ndivyo lakini, kupiga au kuachana baada ya kufumaniana kunasaidia?
Jibu hakusaidii, kwani ukimpiga adhabu inaishia hapo hapo, kesho yake
watakaokutana watakusaliti tena kupozana machungu.
Maamuzi ya kuacha naye hayasaidii kwani ukimwacha mpenzi
wako hujamtibu, utakuwa umetoa mwanya wa yeye kuendelea kukusaliti na
kukuumiza zaidi pale macho yako yatakapowaona wameshikana mikono mitaani
kwa uhuru na raha zao.
Ukiamua kuua na wewe utauawa, huku wanadamu wenzako
wakikucheka kwa uzembe wa kufikiri. Jamani usaliti upo kila siku, si
tunawaona wake na wapenzi wa watu wanaingizana gesti kila siku?
Hivyo, kama hujamfuma mpenzi wako leo kuna siku utakutana
na meseji kali akibembelezana na ‘kidume’ mwingine kwa maeneo fulani.
Utafanyaje baada ya kubaini hivyo, maana kama ni tukio basi utakuwa
umeona lile la stejini laivuuuuuu bila chenga. Twende pamoja ili
tuelimishane kama wadau wa mapenzi njia sahihi ya kufanya ili kumwadhibu
mpenzi msaliti.
Kwanza, baada ya kuwaona uso kwa macho wakisaliti penzi,
unatakiwa kutoa ishara zitakazoonesha kuwa umewaona, halafu ondoka eneo
hilo. Ukifika home mtu mzima endelea kunywa maji ili kupoza presha.
Akirudi mpenzi wako jitahidi kumkaribisha kwa bashasha, lakini
usimuulize ulichoona mwache aendelee kujiuliza mwenyewe.
Au kama umenasa meseji za kimahaba kutoka kwa mwizi wako,
zitume kwenye simu yako kwanza, kisha baada ya kumaliza uchunguzi wako
mtumie tena sms hizo mkeo/mumeo. Ukifanya hivyo usimuulize, endelea
kumpenda na ikiwezekana ongeza matunzo. Nunua ‘mikuku’ akaange kila siku
na umpe penzi moto moto.
Nakwambia ukifanya hivyo mpenzi wako ataumia sana na
hataendelea kukusaliti kwa kuwa atakuwa anawaza unafikiria kumfanya
nini? Na kwa yule uliyemshika naye, vivyo hivyo usizozane naye, mwache!
Utashangaa anahama eneo maana atakuwa anafikiri unamwandalia kombora
kumbe wewe wala, umeamua kujituliza tu!
Wadau wa mapenzi hii ndiyo dawa ya mtu msaliti. Mwadhibu
kwa upole, wanasaikolojia wameithibitisha adhabu hii kuwa ina uchungu
mara 1,000 zaidi ya kupiga au kukemea. Ukisema umwache siyo dawa kwani
unaweza kutafuta mwanamke/mwanaume mwingine naye akawa na tabia zile
zile, ikiwa ndivyo utaacha wangapi basi katika maisha haya?
Adhabu ya mpenzi anayekusaliti ni kumnasa kwenye usaliti
wake kisha kumpuuza huku wewe ukiendelea na mambo yako kama kawaida,
ukifanya hivyo utakuwa unamtibu ugonjwa wake wa kupenda penda hovyo na
hii ndiyo dawa hasa ya kumponya msaliti, lakini pia inasaidia kupunguza
maumivu ya penzi. Kumchunga na kumlilia machozi hakusaidii
No comments:
Post a Comment