MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Tuesday, 14 January 2014

HII INASIKITISHA TAZAMA JINSI WASANII WA BONGO FLAVA WALIVYOKAMATWA NA BANGI JIJINI DAR

Vijana ni nguvu kazi ya taifa, lakini vijana hao hao wanaweza kuwa chanzo cha taifa kutoendelea na kubomoka. Ubomoaji wa taifa huwa kwa namna nyingi ikiwemo uvivu, ufisadi, na kadha wa kadha. Lakini hapa, tuangalie hili la madawa ya kulevya na bangi.

Ferouz (mwenye kofia) akiwa chini ya ulinzi

Kila kukicha kuna wasanii wa maigizo na filamu ambao tunasikia wamekamatwa na madawa ya kulevya, "unga" katika jitihada za 'kusaka maisha', wenyewe wanasema kuna ajali kazini. Wasanii hao ambao wengi ni vijana, na pale wanapoonekana kwenye runinga huwa hamasa kwa wadogo zao na jamii kwa ujumla, wakipenda kuwa kama wao.


Na mchana huu, maeneo ya Sinza, kuna taarifa ya mwanamuziki aliyetamba kwenye muziki wa bongo fleva, Ferouz, sanasana kwa wimbo wake wa Starehe, ambao ulikuwa ukionyesha madhara ya UKIMWI na virusi vya UKIMWI. Ferouz anadaiwa kukutwa na bangi, na picha ambazo Gospel Kitaa imezipata eneo la tukio, zinamuonyesha akisindikizwa na maafande kunako mbele ya vyombo husika.


Vijana wa Tanzania tuna shida gani? Kama ni ardhi tunayo, kama ni nguvu tunazo, sasa nini shida zaidi? Ipo haja ya Operesheni ambazo Askofu Sylvester Gamanywa ameitisha za Takasika iliyomalizika hivi karibuni, na kisha kupokelewa na Operesheni Milikisha, kuwahusisha pia wasanii wa aina zote, maana wanaonekana kukumbwa na janga hili kwa sana, vinginevyo, vijana ambao ndio nguvukazi ya taifa watakuwa wakijaa jela za ndani na nje, wakiacha wageni kuja kutawala.

No comments:

Post a Comment