MATANGAZO
/zest+mkali+3.jpg
/TULAMCHA+2+copy.jpg
Friday, 3 January 2014
BALAAA MUME WA THEA AFUMANIWA NA KIMADA SOMA ZAIDI
MWAKA ulianza vibaya kwa mke wa mtu ambaye jina lake halikupatikana mara moja kumkimbia mumewe na kumfuata mume wa msanii wa filamu, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ aitwaye Michael Sangu ‘Mike’ jambo lililosababisha ale kichapo cha nguvu na kuuanza mwaka mpya vibaya.
Tukio hilo lililovuta hisia za wengi, lilitokea siku ya mkesha wa mwaka mpya, usiku wa kuamkia Jumatano, katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar ambapo Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ ilikuwa ikikonga nyoyo za mashabiki wake.
KAMERA ZA IJUMAA
Paparazi wetu aliyekuwa ukumbini humo alimuona Mike akiwa upande mwingine na washikaji zake huku wakiendelea kula raha wakati wa shangwe za mwaka mpya wakati mdada huyo ‘kibonge’ akiwa na mumewe na watu wengine wakifanya yao.
Ijumaa lilipata shaka kidogo, baada ya kumuona dada huyo akimwacha mumewe kila wimbo unapokolea na kwenda alipokuwa Mike kisha kucheza naye.
Harufu ya ugomvi ilianza kunukia mapema, baada ya paparazi wetu kumshuhudia mume wa dada huyo akionekana kumkaripia japo kwa sauti ndogo mkewe kila aporudi akitokea kucheza na Mike.
ONYO HALIKUZAA MATUNDA
Pamoja na onyo alilokuwa akitoa mume huyo kwa mkewe mara kwa mara, bado dada huyo alionekana kumfuata Mike na kucheza naye tena kwa ukaribu kama vile wanajuana.
Baadaye jamaa huyo aliamua kuwashirikisha marafiki aliokuwa amekaa nao meza moja kuhusu tabia ya mkewe, wakamsihi asiende tena kucheza lakini bado hakusikia.
“Sisi tulimwambia, mwenzako hataki uende kucheza na yule msanii, anahisi labda kuna kitu kinaendelea lakini hakusikia, sijui ni pombe zilimzidi au vipi,” alisema mmoja wa watu waliokuwa wameketi meza moja na wanandoa hao muda mfupi baada ya tukio la kichapo kutokea.
Akaongeza: “Kuna wakati alikuwa akijifanya ameelewa, lakini sasa alikuwa akiaga na kujifanya anakwenda msalani halafu mumewe akifuatilia anagundua kumbe amemfuata Mike ili wacheze, jamaa akachukia sana.”
KICHAPO
Baada ya mume kuona dharau za waziwazi zikifanywa na mkewe mbele ya watu aliokuwa amekaa nao, aliamua kusimama na kumfuata alipokuwa akicheza na Mike.
Hakuwa na haja ya kuuliza chochote, alimkamata mkewe na kuanza kumshushia kichapo cha nguvu huku wengi wakiendelea kuponda raha kama vile hakuna kilichotokea.
“Ni mke wake? Hizo ni dharau, acha apigwe. Hawa wanawake wa Dar ni wajinga sana. Utamwachaje mumeo uende kushobokea wasanii? Huu ni upuuzi. Ni haki ale kichapo,” alisikika akisema jamaa mmoja aliyekuwa jirani na paparazi wetu.
DAMU CHAPACHAPA
Hasira zilipompanda yule jamaa, hakuchagua mahali pa kupiga, alimvuta nywele na kumpiga makonde kila sehemu ya mwili wake hali iliyosababisha damu imwagike chapachapa (angalia picha ukurasa wa mbele).
Mashuhuda walipoona damu imemwagika ndipo wakaingiwa na huruma na kuamulia ugomvi huo.
UTETEZI WA MKE
Katika kujitetea, mwanamke yule alimlaumu mumewe kwa kumpiga hadi kufikia kutoa damu kwa kosa la kucheza na Mike akisema kwamba, haoni kosa lake.
“Mume wangu unanionea tu bure, huyu sina uhusiano naye wowote ule... nacheza naye tu kama marafiki. Simfahamu na wala sijawahi kumuona zaidi ya kwenye filamu,” alisema mwanamke huyo.
MIKE HUYU HAPA
Kwa upande wa Mike, alipoulizwa na mwandishi wetu kuhusu kisanga hicho alisema, anamshangaa jamaa mwenye mke kwa sababu amemuonea mkewe bila sababu ya msingi.
“Kuna kosa gani watu kucheza muziki? Hapa ni ukumbi wa muziki, tena usiku. Hakuna mipaka, yeyote anaweza kucheza na yeyote. Ule mimi naweza kusema ni ulimbukeni wa kutojua mambo.
“Amemuonea... yule dada alikuwa anafurahi tu sherehe za mwaka mpya ambapo staili yake ya kucheza labda imemkera mumewe lakini kama alikuwa hataki mkewe acheze na mtu mwingine, si wangekaa tu chumbani kwao wawashe redio wacheze wawili tu kuliko kuja kuleta kero kwenye kumbi za burudani?” alisema Mike.
Alipoulizwa hajisikii vibaya kucheza na mke wa mtu alijibu kwa kifupi sana: “Kwanza ningejuaje?”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment