Ni funga mwaka! Mastaa wa Kibongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Recho Haule,
Belina Mgeni na Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ wamejikuta wakiumalizia
mwaka 2013 wakiwa ‘vitumbo ndii’ licha ya kuwa bado hawajaolewa,....
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wasanii hao
wamebeba mimba hizo kwa nyakati tofauti na wamekuwa wakijificha kukwepa
aibu ya kubeba ujauzito kabla ya kufunga ndoa.
Belina Mgeni.
“Wanaona aibu kubeba ujauzito kabla ya ndoa, wamekuwa wakijificha na
mbaya zaidi hawataki kujionesha maana wengi wao hawajawatambulisha
wachumba wao kwa wazazi wao,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la
kutotaja jina lake.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mapaparazi wetu
waliingia mzigoni kusaka ukweli wa habari hiyo ambapo jitihada zilizaa
matunda kwa kupatikana kwa picha za mastaa hao zikionesha tayari vitumbo
ndii.
Jennifer Kyaka ‘Odama’.
Baadhi yao, picha zilionesha mimba zikiwa ni kubwa huku wengine
zikionekana ndiyo bado changa.
Aunty Lulu, Belina walionekana dhahiri
kuwa ni waleo au kesho, matumbo yao yalionekana ‘live’ ni makubwa, Odama
yeye ilionekana bado halijajitokeza vizuri.
Recho Haule.
Kwa upande wa Recho Haule, rafiki wa karibu aliyeomba hifadhi ya
jina, alipenyeza habari kuwa mimba aliyonayo shosti wake huyo ni ya
mpenzi wake wa kitambo, Saguda George lakini naye amekuwa akijifungia
ndani kukwepa macho ya watu.
“Recho ni mjamzito lakini amekuwa
akijificha kukwepa kamera za mapaparazi si unajua tena uchumba wake na
Sagunda kila mmoja alikuwa akiufatilia magazetini!”
Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’.
Baada ya mapaparazi wetu kujitosheleza na ushahidi wa picha, zoezi la
kuwasaka wasanii hao ili kujua wahusika wa mimba hizo lakini simu zao
ziliita muda mrefu bila kupokelewa.
Baadhi ya mashabiki walioongea
na paparazi wetu, hawakusita kuonesha hisia zao kwa mastaa hao, kila
mtu alikuwa na mtazamo wake juu ya mastaa hao.
“Unajua kama Belina naona amebeba mimba ila yuko kwenye process ya
kufunga ndoa ingawa sijui ni lini kwani niliwahi kumsikia akisema kuwa
anaweza kufunga ndoa soon” alisema shabiki mmoja, mwingine akasema hivi:
“Sisi tujuavyo kioo cha jamii maana yake ni mtu kufanya yale yanayofaa
kuigwa lakini kwa hawa mastaa wetu wamefanya tofauti, wote wamebeba
mimba bila ndoa, sasa jamii itajifunza nini kutoka kwao?”
No comments:
Post a Comment