MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Tuesday, 10 December 2013

EVERTON RIBEIRO: MCHEZAJI BORA WA LIGI YA BRAZIL ANAYETAMANI KUICHEZEA MAN UNITED

Everton Ribeiro amekaririwa akisema atafurahia kipata nafasi ya kujiunga na Manchester United.
 
United wameonyesha kuvutiwa na Ribeiro ambaye aliisaidia  Cruzeiro kushinda ubingwa wa Brazil na alitajwa kuwa mchezaji bora wa ligi hiyo msimu unaoisha hivi sasa.
 
Ribeiro aliiambia ESPN Brasil: ‘United wana Kagawa, Rooney, De Gea ni golikipa mzuri. Nawajua vizuri kwa sababu ninawauatilia na pia nachezea sana timu hiyo kwenye video games kwasababu ni timu nzuri.  
 
‘Nahisi nipo tayari kucheza popote pale duniani. Ikiwa unachezea Cruzeiro, basi unaweza kucheza popote pale. Naweza katika nafasi yoyote katika eneo la kiungo. Nacheza vizuri pia katika kusaidia mashambulizi.’
 
Alipoulizwa kama atakuwa akicheza pamoja na Robin van Persie na Wayne Rooney, kiungo huyo alisema: ‘Itakuwa jambo zuri sana. Namuachia wakala wangu na  Cruzeiro kuzungumzia juu ya suala hilo. Ikiwa wataona ni jambo la faida kwetu sote, watanifahamisha."
 
Credit Shaffih Dauda
 

No comments:

Post a Comment