Wadau mnaona mambo haya?!!!
Katikati ni Sarah Kalinga ambaye ni Mkurugenzi na mratibu wa Miss Redds 2013 Mbeya Vijijini ambaye pia anaongoza kampuni ya Mama Neema Decoration..
WALIMBWENDE
12 wanatarajia kuwania taji la Miss Redds 2013 katika wilaya ya Mbeya Vijiji mkaoni
hapa, linalotarajia kufanyika katika ukumbi wa Royal Tughimbe Mei 24, mwaka huu
mjini Mbalizi wilayani humo.
Mkurugenzi
na mtaribu wa shindano hilo Sarah Kalinga kupitia kampuni ya Mama Neema
Decoration Interprises, aliliambia Tanzania Daima jana kuwa maandalizi yanaendelea na tayari
warembo wameingia kambini.
Alisema warembo
wote waliojitokeza mwaka huu wana sifa zinazolingana na wanashindwa kuwachuja
tofauti na miaka mingine iliyopita ambapo walikuwa wanakuwa na warembo tisa
katika kambi yao.
Alivitaja
vigezo vya warembo hao kuwa ni elimu, mwonekano, kimo, nidhamu, kujiamini na
kigezo kingine ni kipaji.
‘’Sifa
ambazo zinaweza kumuondoa mrembo kambini na kumfuta katika ushiriki wa
mashindano ni ulevi, matumizi ya simu, kutembelewa na boyfried, wizi, uchafu
na kauli mbaya kwa wenzao na hata wakufunzi wao’’ alisema Sarah.
Alisema
mbali na uhitaji wa wadhamini katika shindano hilo kuanzia sasa ambapo warembo
wapo kambini, baadhi ya wadhamini wamejitokeza wakiwemo TBL, SBC, Mbaspo,Access
Computer, Tuhimbe Hotel, River side Mbalizi, Grace College, Mjasiliamali
Sanga,Overcado Saloon, Royal Berbershop, mtandao wa na Royal Berbershop
Alipoulizwa
changamoto zaidi alisema kuwa ni kukatwa majina ya warembo kutoka wilayani
wanapokuwa katika mashindano ya mkoa kwenda kanda hali ambayo alisema ni vema
ikatazamwa na waandaaji wa ngazi hizo.



No comments:
Post a Comment