Baada ya msanii wa Candy n Candy, Baby Madaha kufunguka akimchana wazi msanii mwenzake wa kike, Shilole kwa kudai kuwa nyimbo zake haziwezi kulinganishwa na nyimbo anazofanya Shilole, Shilole nae kakikalia kiti kile kile na kuyajibu makavu hayo.
Shilole amedai kuwa hawezi kupoteza muda kumzungumzia Baby Madaha, na
kwamba yeye anaamini hana tatizo naye lakini anashangaa kuona
anamzungumzia.
“Ni kama Baby Madaha anavyonizungumzia mimi, mmekua mkiona na wengine
mliumia mkasema sana kwa nini ananizungumzia mimi. Baby Madaha sina
tatizo naye lakini nashangaa amekuwa mtu wa kunizungumzia everyday, I
don’t know why.” Amesema Baby Madaha.
Mkali huyo aliamua kumpa ushauri Baby Madaha kwa kile alichokiita kumsema yeye vibaya ni kupoteza muda wake.
“Wewe mwanamke, mimi mwanamke mwenzio nafanya kazi, umeshaniona hata
siku moja naenda kukuzungumzia somewhere? Muogope Mungu kukaa
unamzungumzia mtu ambaye hana time, hana shida na wewe. Hebu tubadilike
wanawake tupendane tuache kuzumziana vibaya.” Shilole ameeleza.
“Kwani ukinizungumzia mimi vizuri utapata nini, najua kuna vitu vingi
nimekuzidi lakini usikae unamzungumzia vibaya. Wanawake tupendane
tupeane sapoti. Ndio maana hatufiki mahali tunabaki tu kulalamika ‘ooh
nimerogwa’, hujarogwa umejiroga mwenyewe.” Shilole anakaririwa.
Chanzo: Channel 10
No comments:
Post a Comment