Waliofariki walikuwa watu waliokuwa wanatoroka vita Sudan Kusin
Zaidi ya watu 200 raia wa Sudan Kusini wamezama
katika ajali ya boti kwenye mto Nile wakikimbia vita vinavyoendelea
katika mji wa Malakal.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Sudan Kusini.
Boti hiyo iliyozama, ilikuwa imewabeba watu
wengi kupindukia. Watu hao walikuwa wanatoroka vita vinavyotokota katika
mji wa Malakal.
Mapigano yalizuka Sudan Kusini mwezi Disemba
mwaka jana baada ya Rais Salva Kiir kumtuhumu aliyekuwa makamu wake wa
Rais Riek Machar, kwa kuwa na njama ya kumpindua.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 1,000 wameuawa tangu ghasia kuanza nchini humo.
No comments:
Post a Comment