Mariam Ismail
Mastaa wa filamu nchini Mariam Ismail na Irene Uwoya wanadaiwa kuwa na
uhusiano wa kimapenzi(usagaji) na kudaiwa kuishi pamoja kabisa. wiki
kadhaa nyuma muigizaji mmoja chipukizi anayekuja juu kwa kasi aliutonya
mtandao huu kwa kusema " Mariam Ismail na Uwoya wanasagana tena wanaishi
pamoja kabisa, fuatilieni mtajua".
Baada ya habari hizo ilibidi Swahiliworldplanet kuwatafuta mastaa hao, wa kwanza kutafutwa akiwa Irene Uwoya lakini namba yake ya simu kwa takribani wiki 2 ilikuwa haipatikani na hata jana alipotumiwa ujumbe kupitia namba yake nyingine hakujibu.
Baada ya hapo ilibidi kumtafuta Mariam Ismail ambaye wamecheza filamu nyingi na Irene Uwoya kama vile Sobbing Sound, Omega Confusion, The Return Of Omega na Apple, Hata hivyo Mariam anafanya vizuri katika filamu alionekana kuwa busy na kuchelewa kujibu ujumbe wa madai ya kusagana na Uwoya lakini jana star huyo aliyejipatia umaarufu kwa kuuvaa vizuri uhusika katika filamu zake alitoa ushirikiano mzuri kwa kujibu madai hayo akidai sio kweli ila yeye na Uwoya ni marafiki wa karibu sana na wanasaidiana katika shida na raha ndiyo maana baadhi ya watu wameshaanza kusema vibaya...

"Nadhani mimi ndio mtu wa kwanza
kupiga vita upumbavu kama huo... mimi ni mwanamke ambae nimeumbwa
kikamilifu.. sina kasoro yoyote ya kunifanya niwe na mwanamke
mwenzangu....hao wanaofanya upumbavu huo nadhani wana vijikasoro kwenye
mili yao.... Irene Uwoya ni rafiki yangu sana tena urafiki wetu sio wa
leo wala kesho... ni marafiki wa kushibana kabisa... nikoseapo huwa
ananikosoa na yeye akoseapo huwa namkosoa....sometimes huwa tunagombana na
kupatana vitu ambavyo ni vya kawaida katika maisha." alisema Mariam ambaye hajawahi kukumbwa na skendo yoyote ile kabla.
Mariam ambaye kipaji chake cha filamu hujionyesha waziwazi alimalizia kwa kusema "Irene ananiheshimu
sana na mimi humuheshimu sana Irene, imefikia hatua ya mimi na yeye tukakaa
chini na kupanga tuishi wote kitu ambacho sioni tatizo na hilo. Ingekua
ni chumba kimoja hapo sawa... lakini ni nyumba kubwa yenye
kujitosheleza...kila mtu na room yake...tunaishi kwa amani na kwa
kushirikiana penye tatizo hulitatua wenyewe bila kumshirikisha mtu.
No comments:
Post a Comment