Katika mahojiano ‘spesho’ na gazeti hili yaliyofanyika kwenye ofisi za Global Publishers, Bamaga, Mwenge, Dar es Salaam, juzi, Masogange aliamua kumwanika kigogo huyo huku akimtaja jina bila kuuma maneno.
Melisa Edward.
TWENDE PAMOJA Risasi: Masogange
tumekuita leo hapa kwa ajili ya mahojiano maalum. Tangu umerudi Bongo
toka Afrika Kusini ulikokutwa na ule msala wako, naamini hujawahi
kuzungumza na chombo chochote cha habari. Uongo, kweli?Masogange: Kweli kabisa.
Risasi: Risasi linakukaribisha tuzungumze mambo muhimu, lakini kubwa kuliko yote, hebu mtaje mtu aliyekutuma kubeba ule unga ambao ulikamatwa nao Afrika Kusini.
Masogange: (akionesha sura ya umakini) kusema ule ukweli, ni…(anamtaja jina). Huyu bwana ndiye aliyeniponza kwa yote yale.
Risasi: (bila mshtuko baada ya kutajwa kwa jina hilo). Huyo mtu ni Mtanzania kweli?
Masogange: Hapana, ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ila anaishi Tanzania miaka nenda, miaka rudi.
Risasi: Sasa Masogange, huyu mtu ilikuwajekuwaje hadi akakutuma kupeleka mzigo ule Afrika Kusini, hapo pana utata kidogo.
Masogange: Wengi hawajui. Iko hivi, siku ile (Julai 5, 2013) mimi nilikuwa nasafiri kwenda Sauz kwa mambo yangu tu. Nilipofika pale Uwanja wa Ndege (Julius Nyerere International Airpot) nilimkuta huyo mtu.
Risasi: Naye akiwa anasafiri kwenda huko?
Masogange: Hapana. Yeye tunafahamiana kwa muda mrefu, aliponiona aliniuliza kama nakwenda Sauz, nikamwambia ndiyo. Akasema anaomba nimbebee mizigo yake ya sukari.
Nilimkatalia, lakini akasema kuna mtu atanipokea Uwanja wa Ndege (wa Kimataifa wa Oliver Tambo) uliopo (Kempton Park) Johannesburg.
Basi nilimkubalia, lakini…
Risasi: Subiri kwanza Masogange. Hapo una maana wewe kazi yako ilikuwa kubeba tu, baada ya kutua kule ungekutana na mwenye mzigo, Je, uliuangalia mzigo wenyewe kama kweli ni sukari?
Masogange: Ndiyo. Nilimwambia anifungulie nione kama kweli ni sukari, akafungua begi moja, nikachungulia na kuona kweli ni sukari nyeupe!
Nilimwambia kama anataka nimsaidie kuufikisha Afrika Kusini, apeleke mpaka kwenye ndege ili kunipunguzia kazi ya kubebabeba. Nikifika Sauz nitamtolea huyo mtu sukari yake.
Basi, akapeleka mpaka kwenye ndege, mimi nikapanda na safari ikaanza.
Risasi: Subiri kidogo Masogange. Wewe ulikamatwa na mtu anayedaiwa ni ndugu yako, Melisa Edward. Mbona humtaji?
Masogange: Oke, yule tulikuwa safari moja tu. Lakini yule Mkongomani anajuana na mimi.
Risasi: Oke, endelea.
Masogange: Tulifika uwanja wa ndege salama. Nikashuka na yale mabegi nayo, lakini cha ajabu wakatokea askari na kutukamata.
Waliniuliza nimebeba nini? Nikawaambia sukari, wakasema siyo sukari, wakanitaka nilambe. Kulamba hivi, ndiyo nikajua kweli siyo sukari, tukawekwa chini ya ulinzi na kupelekwa kwenye vyombo vyao vya sheria kwa hatua zaidi.
Risasi: Pole sana. Kwa hiyo yule mtu ambaye angepokea mzigo kule Sauz ulimwona ulipotua uwanjwa wa ndege?
Masogange: Sikuwa namjua kwa sura, nilipewa mawasiliano yake tu. Kuna uwezekano alituona wakati tumekamatwa na polisi maana tulizungukwa na watu wengi.
Risasi: Unakumbuka yalikuwa mabegi mangapi ya hiyo ‘sukari’?
Masogange: Hata sikumbuki vizuri mimi, nilishachanganyikiwaga jamani, yalipita yale. Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari kwa kuwaonyesha picha ya Agnes Gerald ‘Masogange’ katika simu ya samsung Tab.
ANAYEMJUA MWAKYEMBE
Siku chache baada ya mlimbwende huyo kunaswa Sauz, Bongo, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George Mwakyembe alimtaja kijana ajulikanaye kwa jina moja la Mangunga kwamba ndiye aliyedaiwa kuwa na video queen huyo ndani ya ndege kwenda Afrika Kusini.
Kamanda
Nzoa aliwataja wanawake hao baada ya kukamatwa kuwa ni Agnes Jerald
ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 na
Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989.
Mwakyembe aliamuru kijana huyo asakwe na kukamatwa ili kujibu
mashitaka ya kusafirisha madawa ya kulevya aina ya Methamphetamine kwa
Tanzania huku Sauz ikisema ‘unga’ huo ni ephedrine ambao si wa kulevywa
bali ni malighafi haramu.
Nassoro.
Masogange na mwezake, Melisa walikamatwa Julai 5, mwaka jana kwenye
uwanja huo wa ndege nchini humo wakiwa na madawa hayo yaliyokadiriwa
kuwa na thamani ya shilingi bilioni 6.8.Kesi yake iliendeshwa na Mahakama Kuu ya Gauteng iliyopo Kempton Park nchini humo na alikutwa na hatia ambapo alihukumiwa kwenda jela miezi 32 au kulipa faini ya randi 30,000 (shilingi milioni 4.8). Masogange alilipa faini huku mwenzake, Melisa akiachiwa huru kukutwa hana hatia.
No comments:
Post a Comment