MKALI
wa muzi Bongo Kala Jerimiah "Kala" amesema kwamba msanii nyota wa kike
wa Bongo movie Wastara Juma "Wastara" ndiye mwenye sifa zote za mwanamke
ambaye anahitaji kuishi naye.
Kala aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita alipoongea na mwandishi wa habari hizi na kuongeza kwamba kila awazapo suala la kuwa na mke basi mawazo yake huenda kwa Wastara kwa kuminganisha na sifa zake.
"Siyo Siri, Wastara ndiye mwenye sifa za kuwa mke wangu mtarajiwa. Si kwamba namtaka yeye hapana ila nahitaji mwanamke mwenye sifa kama zake. Namkubali sana Wastara. Napiga picha jinsi alivyovumilia kwa mengi. Ndoa yake na marehemu Sajuki ilikumbana na changamoto nyingi sana. Mpaka sasa amekomaa bila kuolewa na maisha yanasonga kama kawaida. Dah! kwa kweli nikipata mke kama huyu nitafurahi sana japo wapo wachache sana Duniani" Alisema Kala Jeremiah.
Akieleza ni kwanini amefikia hatua ya kuzungumzia suala la ndoa na kama anampango wa kuoa, Kala alisema kwamba yeye ni mwanaume mwenye sifa zote za kuoa na ni lazima ataoa hivyo si ajabu kuzungumzia suala hilo.
No comments:
Post a Comment