OPARESHENI ya Polisi wa Mkoa wa Morogoro na kikosi maalum cha
kufichua Maovu cha Magazeti ya Global Publishers (OFM), imemnasa
mwanamke mjamzito katika kamatakamata ya machangudoa.
Katika oparesheni hiyo ya aina yake iliyofanyika mwishoni mwa wiki
iliyopita katika eneo la Msamvu (Kambi ya Itigi), wanawake 30 waliodaiwa
kujihusisha na biashara hiyo walikamatwa.
Waandishi wetu wakiwa na askari wa mkoa huo walimnasa mjamzito huyo anayedaiwa kuwa na mimba ya miezi sita akiwa mawindoni eneo hilo.
Waandishi wetu wakiwa na askari wa mkoa huo walimnasa mjamzito huyo anayedaiwa kuwa na mimba ya miezi sita akiwa mawindoni eneo hilo.
Changudoa huyo mwenye mimba akiwa chini ya ulinzi.
Mara baada ya mjazito huyo kukamatwa alitoa yake ya moyoni kwa kusema
kwamba anafanya biashara hiyo ili kupata fedha za kujikimu na ujauzito
wake haumpi shida yoyote.
“Jamani natafuta pesa za kujikimu na maisha hapa mjini sasa mnatukamata tukale wapi? Hii mimba ni yangu na ninayefanya ukahaba ni mimi niacheni,” alisema mdada huyo
“Jamani natafuta pesa za kujikimu na maisha hapa mjini sasa mnatukamata tukale wapi? Hii mimba ni yangu na ninayefanya ukahaba ni mimi niacheni,” alisema mdada huyo
No comments:
Post a Comment