Mwishoni mwa wiki iliyopita, operation
fichua maovu, OFM ilitua ‘Mji Kasoro Bahari’ (Morogoro) ambapo kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi Morogoro, kazi kubwa ilifanyika.
KAZI YENYEWE
Kazi ilikuwa kuyafumua madanguro na maeneo ya kujiuzia makahaba ambapo kwa mujibu wa watoa habari, baadhi ya maeneo mjini humo (hatuyataji kwa sasa) yamekubuhu kwa biashara ya wanawake kuuza miili yao.
MAENEO YALIYOFIKIWA NA OFM
OFM na jeshi la polisi walijipanga sawa kwa ushirikiano huku wakitumia mbinu za hali ya juu ili kuwanasa machangu hao.
Itigi Msamvu ni kambi maarufu ya
machangudoa hao ambapo wateja wao wakubwa ni baadhi ya madereva wa
magari makubwa ‘malori’ wanaoegesha magari yao eneo hilo lililopo
kandokando ya Barabara Kuu ya Morogoro -Dar es Salaam.
ILIKUWAJE?
Awali, wakazi wa eneo hilo walilalamikia uchafuzi wa mazingira na hatari kwa watoto wao kupata magonjwa ya ajabu kutokana na utupwaji hovyo wa kondom zilizotumika unaofanywa na machangu hao ambapo watoto hao huziokota na kuzigeuza maputo.
Wakazi hao walisema kuwa wamesharipoti hali hiyo kwa jeshi la polisi lakini kulionekana kusuasua.
Mbali na athari za mwanzo, wakazi hao waliwaambia OFM kuwa, kumekuwa na tabia ya ukabaji na unyang’anyi kwa watu ambao wanakatisha katika vichochoro vya eneo hilo.
Mbali na athari za mwanzo, wakazi hao waliwaambia OFM kuwa, kumekuwa na tabia ya ukabaji na unyang’anyi kwa watu ambao wanakatisha katika vichochoro vya eneo hilo.
MSIKIE HUYU
“Jamani OFM tunaomba msaada wenu kwani hapa Msamvu ni jehanam, maasi yote yanafanyika hapa, ngono mpaka kwenye uvungu wa magari makubwa ambayo yamepaki, watu wanakabwa, kondom zilizotumika zimezagaa hovyo,” alisema mkazi mmoja aliyesema anaitwa Mkude.
OFM NA JESHI LA POLISI
Baada ya kupokea malalamiko hayo, OFM waliwasiliana na jeshi la polisi mkoani hapo ambapo walisema wapo katika kujipanga kuingiza operesheni ya kufungua mwaka 2014.
”Ni kweli kabisa wakazi wa hapo
wanapalalamikia sana pale mahali lakini tumeshajipanga, hata RPC
nadhani alishawaambia nyie (OFM) mje mshuhudie kazi. Tena kama mnaweza,
leo si Alhamisi (Januari 9, 2014) kesho Ijumaa njooni tuingie kazini,
sisi hatuna siasa,” alisema afisa mmoja wa polisi.
SIKU YA TUKIO
Siku ya tukio ambayo ilikuwa usiku wa saa tano, Ijumaa iliyopita, Kaimu Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Morogoro, Jamal Ibrahim na msaidizi wake wa karibu, Tausi Mbalamwezi huku OFM wakiwa kwa ukaribu nao, walipafungia kazi mahali hapo.
Oparesheni ilifanyika na kufichua maovu
mengi, madada poa kibao walidakwa wakiwa na watu waliojitambulisha kuwa
ni madereva wa malori.
Katika sakata hilo, baadhi ya madereva
ambao ndiyo wateja waliingia mitini, wengine kujifungia kwenye magari
yao na kuwaacha machangudoa hao wakiwa hawana pa kukimbilia na hivyo
kunaswa kama ndege kwenye mtego wa mti wenye ulimbo.
Baadhi ya makahaba walikiri kuliwa uroda na madereva, wakasema ni wateja wao wa siku nyingi na ndipo wanapoponea wao.
“Jamani tunatubu lakini hao madereva
ndiyo wateja wetu wakubwa. Wakija kama hivi kutoka Dar wanakuwaga na
hela sana,” alisema changudoa mmoja bila kujitaja jina.
HA! HATA WAKE ZA WATU!
Katika hali ambayo haikutarajiwa, makahaba wawili walidai wao wameolewa lakini waume zao wapo nje ya mji kikazi ndiyo maana waliamua kujiuza ili kupata ‘chochote’.
UTETEZI WA MADEREVA
Baadhi ya madereva waliozungumza na paparazi wetu walikiri kuwa kuna madereva wenye tabia hiyo ya kuwanunua machangudoa lakini si wote.
“Jamani kwanza tuwekane sawa, si madereva wote wana tabia ya kununua machangu, sisi wengine tunajiheshimu sana, hatuwezi,” alisema dereva mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mafongo baada ya kukutwa pembeni ya lori.
OFM IKAINGIA GESTI
Baada ya polisi kuwasomba makahaba hao wa kwenye malori, OFM na polisi wakaenda kuvamia gesti moja inayojulikana kwa jina la Itigi ambapo, katika hali ya kushangaza, wanawake wawili, mmoja bonge, walinaswa ndani ya chumba kimoja, kitanda kimoja.
Hawakuwa na la kujitetea lakini pembeni
ya kitanda hicho palikuwa na kondom kibao. Watoa habari walisema kuwa,
wanawake hao wamekuwa wakilala humo kwa ajili ya kusaka wateja ambao
huwaingiza ndani ya chumba hicho ‘kuwahudumia’.
Wanawake hao waliunganishwa na wenzao kwenye gari na kupelekwa kituo kikuu cha polisi cha mjini Morogoro.
-CREDIT: GPL VIA OFM
No comments:
Post a Comment