Maumivu anayoyapata Rehema Chalamila aka Ray C ambaye aliwahi kuteseka
na athari kubwa za madawa ya kulevya yanazidi kumsukuma kuwaandama zaidi
wauza unga licha ya kutahadharishwa kuwa anaweza kuuawa na watu hao.
Siku kadhaa baada ya kuandika ujumbe unaosapoti kukamatwa kwa Jacky Cliff nchini China na madawa ya kulevya aina ya heroin huku akipendekeza adhabu ya kunyongwa/kifo kwa watu kama hao, Ray C amepost kwenye instagram picha inayoonesha karatasi lililoandikwa ujumbe unaowashambulia watu waliokamatwa na dawa za kulevya na kuwaita wauaji.
“Pole sana dada yangu. Pole kwa familia yako. Ila hii haitoshi. Itatosha vipi ikiwa vijana wengi wangepoteza muelekeo kama zile dawa zingefika kwa wahusika? Tunaushahidi gani kama dawa alizotumia Ray C hazijaingizwa na wao?” inasomeka sehemu ya ujumbe huo.
Follower mmoja anayetumia jina la mahambakhaleed kwenye instagram aliandika ujumbe wa kumuonya Ray C, “Mchuchu haya mambo ya madawa punguza kuyaongelea wasije kukuua bure wahusika…mi naogopa mwenzio bhana.”
Ray C alionesha kutoshituliwa na vitisho vya kuuawa ambavyo vinaeleweka zaidi kwenye huo mkondo wa madawa ya kulevya.
“Wameuwa wangapi wangu waache waniue kwani si walishaua maisha yangu Na sasa ndo kwanza nachechemea naanza upyA????
hatA wakiniua wao pia iko siku wAtAkufa tu!!!!Mungu kaninusuru ili nirudi kuwasaidia wengine wasithubutu kuyagusa Na waliogusa wayaache!!!kamwe sitanyAmaza mpk naingia kaburini.

No comments:
Post a Comment