Kwa
mujibu wa Abiria waliohojiwa wanasema Boti ya Kilimanjaro II ikitokea
Pemba kuelekea Unguja imepigwa na dhoruba leo Jan 5 2014 kwenye saa nne
asubuhi na kuponea kuzama ilipokua kwenye eneo hatari la Nungwi ambapo
ilizama kidogo mbele na kunyanyuka hivyo watu wa mbele wote wakaachwa
lakini pamoja na kuwatupa hao watu kwenye maji Nahodha akafanya uamuzi
mwingine mgumu.
Aliona
akisimama ili kuwaokoa wale watu boti yote ingezama pale hivyo akaamua
kuendelea na safari lakini kabla ya kuondoka watu kadhaa ndani ya boti
wakajitolea kuwatupia life jacket wale waliotupwa kwenye maji ambapo
shuhuda anasema kama mtu hajui kuogelea anaweza kupoteza maisha kwa
sababu hawakua wamejiandaa kwenye tukio hili la ghafla na sio wote
wamepata vifaa hivyo vya kujiokoa.
Shuhuda
mmoja anasema ‘yani boti ilizama ghafla mbele hivyo watu wakatupwa
kwenye maji kwenye hii sehemu ambayo kuna mkondo wa maji, upepo ulikua
mkali sana yani unaona watu wanajaribu kujiokoa mabegi na vitu vingine
vinaonekana juu ya maji’
Hali ilivyo ndani ya boti ambayo imeendelea na safari ni watu kujawa na huzuni na wengine wamebaki wanalia tu.
KAULI YA POLISI KUHUSU TAARIFA YA ABIRIA 10 WALIOTUPWA MAJINI
Kuhusu taarifa za watu 10 kurushwa baharini wakati upepo mkali ulipotokea, Polisi wanasema ‘hakuna mtu yeyote aliedondoka baharini na hizi taarifa ni kwa mujibu wa Captain wa boti hii N. Abubakar’

No comments:
Post a Comment