MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Wednesday, 29 January 2014

BALAA MREMBO ANUSURIKA KUFA KISA WIZI WA SIMU

MREMBO mmoja mkazi wa Mabibo Makutano jijini Dar es Salaam (jina lake halikupatikana) mwishoni mwa wiki iliyopita alinusurika kifo baada ya kuvamiwa na kudundwa baada ya kudaiwa kukwapua simu ya mwanaume na kuificha sehemu zake za siri.


Mrembo akiwa chini baada ya kuchezea kichapo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, awali mrembo huyo alikuwa akila bata na mwanaume aitwaye Hashim kwenye Baa ya Jassun Inn iliyopo maeneo ya Mabibo huku mwanaume huyo akiwa ametandaza simu zake za kisasa juu ya meza.

Imedaiwa kuwa wakati wakiendelea kuponda raha, Hashim alikwenda msalani kwa lengo la kujisaidia na kuacha simu zake mezani, aliporudi hakumkuta mrembo aliyekuwa akiponda naye raha na simu yake moja haikuwepo.


...Akiwa amewekwa mtu kati na wananchi.
“Jasho lilimtoka Hashim na kuwauliza watu waliokaa jirani alikoelekea mrembo huyo,” alisema shuhuda mmojawapo wa tukio hilo na kubainisha kwamba msamaria mwema mmoja alimweleza Hashim mwelekeo wa mrembo huyo.

Bila kuchelewa Hashim aliwakusanya wapambe wake na kuanza kumtafuta mrembo huyo na wakamnasa mita kama 150 kutoka Baa ya Jassun na kumuuliza kuhusu simu iliyokuwa mezani lakini alileta ubishi.

Walijitahidi sana kumbembeleza ili aitoe simu kwa hiyari yake lakini alikataa, ndipo Hashim na wapambe wakamwanzishia songombingo la nguvu na kufikia kumvua nguo hadharani na simu ikakutwa kwenye nguo yake ya ndani,” shuhuda wetu alisema.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kwamba, hadi kufikia kupatikana kwa simu hiyo, mrembo huyo alikuwa hoi kutokana na vurugu aliyofanyiwa na wapambe wa Hashim ambao walipoipata simu walimvisha nguo pamoja na wigi lake lililokuwa limemvuka.

No comments:

Post a Comment