HAWA NDO NYOTA KUTOKA AFRICA WANAOLIPWA PESA NYINGI KWA KUCHEZA MPIRA
Kutoka
katika orodha iliyotolea na Forbes kuonyesha wanamichezo matajiri zaidi
duniani ikiwa na wanamichezo kama vile Tiger Woods kama mwanamichezo
anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani - dola milioni 78.1 kwa mwaka,
akifuatiwa na mcheza Tennis Roger Federer katika nafasi ya pili na Kobe
Bryant katika nafasi ya tatu, Na sasa pia imefahamika ni wanasoka gani
kutoka Afrika ambao wanalipwa
Hii
ndiyo ile orodha iliyotolewa na Forbes hivi karibuni kuonyesha wasakata
kabumbu kutoka Afrika ambao wanavuna mulla ama pesa ndefu zaidi katika
kazi yao hii kutoka katika clabu mbalimbali wanazochezea. Kwa
kuanzia, katika list hii, wa kwanza kabisa ni mkali Yaya Toure, Raia wa
Ivory Coast ambaye anacheza soka katika clabu ya Machester City, Kwa
mwaka anaingiza Dola milioni 18.2, na mshahara wake wa wiki ni dola
320000 ambayo nnje ya bonus na allowance nyingine.
Yaya Toure
Katika
nafasi ya pili yupo Samuel Eto’o kutoka Cameroon, Staa huyu anakipiga
katika Clabu ya Anzhi kwa sasa, na mshahara wake kwa mwaka ni dola
milioni 13.4, kwa wiki mshahara wake ni dola 300,000.
Eto'o
Wa
tatu ni Didier Drogba wa Ivory Coast, kwa sasa yupo na clabu ya
Galatasaray na mshahara wake kwa mwaka ni dola milioni 12.9, mpunga
anaochukua kwa wiki ni dola 185,000 na pia nnje ya soka huyu ni star
ambaye ana deals mbalimbali za matangazo na kampuni kama Pepsi, Nike,
Samsung na Mtandao wa Orange Ufaransa.
Drogba
Mwingine ni Seydou Keita wa Mali ambaye anasakata kabumbu na clabu ya Dalian Aerbin, Mshahara wake kwa mwaka ni dola milioni 12.
Keita
Anayefuatia
ni Emmanuel Adebayor kutoka Togo, Mshahara wake kwa mwaka ni dola
Milioni 10, Mshahara wake kwa wiki ni dola 220,000, mbali na soka pia
mchezaji huyu ana deals kadhaa za matangazo ambazo zinamuongezea mulla.
No comments:
Post a Comment